POLISI DAR YAPIGA MARUFUKU KUCHOMA MATAIRI NA KUPIGA BARUTI BILA VIBALI

………..

Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharia wananchi wenye tabia
ya kuchoma matairi barabarani na maeneo mengine hatarishi, kupiga baruti au
fataki bila vibali maalum na kwa kufanya hivyo hatua za haraka za kisheria
zitachukuliwa dhidi ya mtu au kundi lolote litakalobainika kufanya vitendo
hivyo na kusababisha hofu au usumbufu kwa jamii.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesema Jeshi la Polisi lina jukumu la
kuzuia na kudhibiti vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya Mwaka Mpya, kwa kushirikiana na vyombo
vingine vya ulinzi na usalama.

Aidha,amesema kuwa Jeshi hilo  litaendelea kushirikiana kwa karibu na
wananchi pia viongozi wa nyumba za ibada ili kuhakikisha usalama unakuwepo
kwenye nyumba za ibada na maeneo mengine.

Kamnda
Muliro amesema Jeshi linaendelea kukumbusha maeneo ya makazi, ofisi na yale
maeneo ya biashara kutoachwa wazi bila uangalizi katika kipindi cha sikuku na
nyakati zingine, Polisi Dar es salaam inawatakia kila la kheri na kusherehekea
kwa amani.