MWENYEKITI CHA CHA NCCR MAGEUZI ATUMA SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026

Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha NCCR Mageuzi Haji Ambar Khamis.

……….

Chama cha siasa cha NCCR Mageuzi kimetuma salamu za mwaka mpya 2026 kwa watanzania na kuwashukuru wote walikiunga mkono Chama hicho katika harakati za kisiasa kwa mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa leo na Mwenyekiti wa chama hicho Haji Ambar Khamis pia amewaomba watanzania kuendelea kukiunga mkono Chama hicho mwaka 2026 huku nao wakiendelea kutekeleza wajibu wao wa kisiasa na hasa kipindi hiki cha kufanya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa na muafaka wa kitaifa.

Aidha Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa watanzania wote na wapenda amani kutokana na tukio lililotokea tar 29 Oktoba,2025.

“Tunao ndugu na jamaa ambao walitamani tungekuwa nao leo lakini kwa mapenzi ya MwenyeziMungu hatuko nao tuendelee kuwaombea mapumziko mema”amesema Mwenyekiti Haji 

Amemuomba MwenyeziMungu aendelee kuwa Nguzo yetu sambamba na kutakiana mema ,Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.