Uchizi Vunga  azigonganisha mbili Bara

KIUNGO mshambuliaji wa Silver Strikers ya Malawi, Uchizi Vunga ameziingiza vitani Singida Black Stars na TRA United ambazo zinawania saini yake.

Uchizi ni kiungo ambaye alionyesha ubora dhidi ya Yanga kwenye mechi za hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika na kuibuka gumzo kutokana uwezo aliouonyesha.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Singida Black Stars kimeliambia Mwanaspoti kuwa, ni kweli wameanza mazungumzo na kiungo huyo ambaye wanaamini anaweza kuwa msaada kikosini kwao.

“Baada ya kuondoka kwa Marouf Tichakei nafasi ya kiungo licha ya uwepo wa Clatous Chama bado tunahitaji kuongeza nguvu ili kuwa na uwiano mzuri kutokana na uwepo wa mashindano mengi mbele yetu,” kilisema chanzo.

KISA 03

“Uchizi ni mchezaji ambaye tayari ana uzoefu, ameshashiriki michuano mikubwa, hivyo kama dili lake litaenda kama tulivyokubaliana tunaamini atakuja kuongeza chachu ya ubora na ushindani eneo analocheza.”

Chanzo hicho kilisema usajili unaofanywa ni mahitaji ya benchi la ufundi baada ya tathmini iliyofanywa katika mechi chache ilizocheza timu na linatakai kuboresha na kuongweza nguvu kikosini ili kurudi katika mashindano timu ikiwa shindani.

KISA 04

Wakati Singida Black Stars ikipambana kukamilisha dili hilo, inaelezwa kuwa TRA United inapambana kupata saini ya mchezaji huyo.

TRA United ambayo ipo chini ya kocha Etienne Ndayiragije inaendelea kuboresha kikosi ili kurudi ikiwa bora na kuendeleza ushindani.