Rais Mwinyi awaachia huru wafungwa 17 maadhimisho miaka 62 ya Mapinduzi

Unguja. Katika kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewaachia huru wafungwa 17.

Hiyo ni kwa mujibu aliopewa chini ya  kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 cha kutoa msamaha kwa mtu aliyehukumiwa kosa lolote.

Katika msamaha huo, jumla ya wafungwa 17 waliokuwa wakitumikia adhabu zao gerezani wameachiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo Januari 11, 2026, na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Raqey Mohamed, imeeleza kati ya wafungwa hao 11 ni wa Unguja na sita ni wa  Pemba.

Hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida kwa Rais kutoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa kwenye maadhimisho ya kitaifa kama haya.

Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea Januari 12, 1974 lengo likiwa ni kuondoa utawala wa mkoloni na kuweka mamlaka mikononi mwa Waafrika.