ZIARA YA WAZIRI MKUU KIDETE NA TINDIKA KILOSA YAACHA NEEMA YA MAJI

FARIDA MANGUBE, MOROGORO
ZIARA ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba katika kata za Kidete na Tindika imekuwa faraja kubwa baada ya Serikali kutoa shilingi milioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji itakayoboresha maisha ya wakazi wa maeneo hayo
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Sospeter Lutonja, amesema kwa Kata ya Kidete vitachimbwa visima 6 vyenye thamani ya shilingi milioni 360, ambavyo vinatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakazi 15,000.
Kwa upande wa Kata ya Tindika, serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika vijiji vya Tindiga A, Tindiga B, na Maluwi ambapo awali wakazi wa maeneo hayo walikuwa wakitumia visima vya mkono maarufu kama “visima vya mdundiko,” ambavyo havikutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.
Ziara ya Waziri Mkuu inaonesha wazi jinsi serikali inavyolenga kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi, hasa katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko na uhaba wa maji safi.