KIHONGOSI AFANYA KIKAO KAZI NA VIONGOZI,WASANII BENDI YA TOT

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Halmashauri Kuu(NEC)ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenan Kihongosi amefanya kikao kazi na viongozi mbalimbali wa Chama hicho pamoja na wasanii wa Bendi ya TOT.

Kihongosi amefanya kikao kazi hicho leo katika Ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi(CCM) zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam ambapo katika kikao hicho ametumia nafasi hiyo kuelezea mipango na mikakati mbalimbali yenye lengo la kuiimarisha Chama hicho.

Aidha Kenan amewahakikishia viongozi walioshiriki kikao kazi hicho kwamba anatambua kazi kubwa na nzuri ambayo wameifanya kipindi chote cha kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025 napia kwa lengo la kukifanya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwatumikia wananchi ambao wamekuwa na matumaini makubwa na Chama hicho chini ya Mwenyekiti wao Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.