Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita (Kushoto) Meneja Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu Agapiti Paul (kulia) na viongozi wengine katika uzinduzi wa miradi inayotekelezwa katika shule ya msingi Segese

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita (Kushoto) Meneja Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu Agapiti Paul (kulia) na viongozi wengine katika uzinduzi wa miradi inayotekelezwa katika shule ya msingi Segese

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mhita (Kushoto) Meneja Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu Agapiti Paul (kulia) na viongozi wengine katika uzinduzi wa miradi inayotekelezwa katika shule ya msingi Segese


Muonekano wa nyumba ya mlezi wa wanafunzi

Muonekano wa ukuta wa shule

Muonekano wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum
*
-Kupitia fedha za CSR yafanikisha ujenzi wa uzio wa shule na nyumba ya matroni
Moja ya changamoto kubwa ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikileta adha kwa jamii na kusababisha watoto wengi kukosa elimu nchini ni uhaba wa madarasa na kutokuwepo miundombinu bora ya elimu kuanzia shule za msingi hadi sekondari.
Hata hivyo Serikali imekuwa ikipambana kuhakikisha inatatua changamoto hii ili watoto wengi wa kitanzania wapate elimu katika mazingira bora kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mfano kampuni ya Barrick inayoendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals na dalili za mafanikio zimeanza kuonekana kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga katika shule za msingi na sekondari.
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia fedha za CSR umetekeleza miradi mingi ya elimu mkoani Shinyanga mojawapo ukiwa ni mradi wa ujenzi wa uzio na nyumba ya mlezi wa wanafunzi (matroni) katika shule ya msingi yenye watoto wenye mahitaji maalum ya Segese iliyopo kwenye halmashauri ya wilaya ya Msalala kwa gharama ya shilingi milioni 238, huku ujenzi wa nyumba ya mlezi ukigharimu shilingi milioni 79.2.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali mkoani humo alitembelea na kukagua ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba ya mlezi (matroni) katika Shule ya Msingi Segese, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Miradi hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 490 na inalenga kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa kundi hilo muhimu katika jamii.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo, Mkuu wa Mkoa ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na wadau kama Barrick, hususan kwa watoto wenye mahitaji maalum, akisema miradi hiyo itasaidia kuongeza usalama, malezi bora na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi hao.
Ujenzi wa bweni la wanafunzi umegharamiwa kupitia fedha kutoka Serikali Kuu pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Frank Nkinda ameshukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Elimu na kuwataka kuitunza na kuitumia vyema ili iweze kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bi. Rose Manumba amesema ataendelea kuhakikisha miradi inasimamiwa vyema na kukamilika kwa wakati katika Halmashauri hiyo kusudi wananchi waweze kupata huduma bora na nzuri.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Mkuu wa Shule ya Msingi Segese, Bw. Alpha Matambo, amesema ujenzi wa majengo hayo utachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza usalama, uangalizi na malezi bora kwa watoto wenye mahitaji maalum, tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza ari ya wanafunzi kuhudhuria masomo na kuwapa wazazi na walezi imani ya kuwapeleka watoto wao shule katika mazingira salama na rafiki.
Kwa upande wake Meneja Mahusiano ya Jamii wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Agapiti Paul amesema kuwa mradi huu n moja ya miradi mingi inayotekelezwa kwa fedha za CSR zinazotolewa na Mgodi katika maeneo ya vijiji vinavyozunguka mgodi inayoendelea kuwanufaisha wananchi.
“Mgodi utaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha miradi ya CSR iliyoibuliwa na wananchi inatekelezwa kwa viwango na kuboresha maisha ya wananchi”, amesema Agapiti.
Kutokana na kuendelea kuimarika kwa miundombinu ya elimu kumewafanya watoto wanaosoma shuleni hapo kuoneana kuwa na furaha na nyuso za matumani ya kupata mafanikio katika safari yao ya elimu na kutimiza ndoto zao.
Barrick ni kampuni kubwa iliyowekeza katika uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini kupitia migodi yake ya North Mara,Bulyanhulu na Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa na inazo programu madhubuti za kuunga mkono za kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha sekta mbalimbali hususani elimu,afya,kuboresha miundombinu na mazingira kwa lengo ya kuboresha maisha ya wananchi.