Dar es Salaam. Mbunge viti maalumu aliyekuwa akiwakilisha kundi la Wafanyakazi wa Sekta binafsi na Umma, Halima Idd amefariki dunia leo Jumapili, Januari 18, 2026 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo hicho zimetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa mazishi ya mbunge huyo yatafanyika leo kwenye makaburi ya Kibada kwa Dole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi