MBUNGE HALIMA NASSOR AFARIKI DUNIA

…….

Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu (Mb) ametangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Halima Idd Nassor, kilichotokea leo Jumapili tarehe 18 Januari, 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu,

Taarifa iliyotolewa na @bunge.tanzania imeelezakuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

“Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mbunge wa Viti Mheshimiwa Halima Idd Nassoro kilichotokea leo 18 Januari,

2026 Jijini Dar es Salaam,

Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, famillia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika