Manyoni, Singida, Januari 18, 2026
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Kenani Labani Kihongosi, ameanza rasmi ziara yake ya kimkakati leo tarehe 18 Januari 2026 mkoani Singida, ambapo ameanzia Wilaya ya Manyoni.
Ziara hii ni ziara maalum ya Chama Cha Mapinduzi inayolenga kuhakikisha Chama kinawafikia wanachama wote nchini sambamba na kusikiliza kero za wananchi, kuzifanyia kazi na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.
Akizungumza na wanachama walio jitokeza, Ndugu Kihongosi aliwasilisha salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alisisitiza umuhimu wa umoja, mshikamano na upendo.
.jpeg)

