Kipa wa Taifa Stars Hussein Masalanga Atua Yanga



Klabu Yanga leo Jumapili, Januari 18, 2026 imetangaza kukamilisha usajili wa kipa Hussein Masalanga akitokea klabu ya Singida Black Stars.

Masalanga aliisaidia Taifa Stars kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza na kuandika historia ya kuwa golikipa wa kwanza kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON akiwa na Taifa Stars.

Masalanga ametambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Yanga, ambapo klabu hiyo ilimkaribisha kwa maneno:

“KIPA LA AFCON @hussein_masalanga ni .”