
Dakika 90 za mchezo wa kukatana shoka kati ya Simba SC na Mtibwa Sugar zimekamilika kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, huku timu hizo zikigawana pointi baada ya sare ya bao 1–1.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mpanzu aliyefunga katika dakika ya 18, na kuwapa wekundu hao uongozi wa mapema. Hata hivyo, Mtibwa Sugar hawakukata tamaa; walirejea mchezoni kwa nguvu na kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Magata.

Licha ya juhudi za pande zote mbili kutafuta bao la ushindi katika dakika zilizobaki, hakuna timu iliyofanikiwa kubadili matokeo, hivyo mchezo ukaisha kwa sare ya haki ya 1–1.

