MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA VIJIJINI MATATANI KWA UCHOCHE

:::::::::

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetangaza kumkamata na kumshikilia Bi. Getruda Japhet Lengesela, Mkazi wa Nsalala- Mbalizi na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Ijumaa Januari 23, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Benjamin Kuzaga imesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana Januari 22, 2026 saa tatu usiku eneo la Nsalala, Mji mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwa ni pamoja na uchochezi.

Kulingana na Polisi, upelelezi unakamilishwa na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yake mara baada ya upelelezi kukamilika.