Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent wakati akizungumza leo tar 23/1/2026 kwenye kikao cha kawaida cha waingizaji na
wazalishaji wa mbolea nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Mamlaka.
Wiliam Ngeleja Mjumbe wa Bodi, Kiwanda cha Mbolea Itracom akizungumza kwa niaba ya wadau wa tasnia ya mbolea leo tar 23/1/2026 kwenye kikao cha kawaida cha waingizaji na wazalishaji wa mbolea nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka.
wadau wa tasnia ya mbolea leo tar 23/1/2026 kwenye kikao cha kawaida cha waingizaji na wazalishaji wa mbolea nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka (picha na Mussa Khalid)
………………..
Mamlaka ya Udhibiti wa
Mbolea Tanzania (TFRA) imewahakikishia wakulima nchini upatikanaji wa mbolea ya
kutosha katika msimu wote wa kilimo wa mwaka 2025/2026.
Mkurugenzi Mtendaji wa
(TFRA) Joel Laurent, ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa
kikao cha kawaida cha waingizaji na wazalishaji wa mbolea nchini,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo.
Amesisitiza kuwa TFRA inaendelea kusimamia kwa karibu upatikanaji, ubora na
usambazaji wa mbolea ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati na
kwa bei himilivu.
Laurent amesema kwa
msimu huu wa kilimo, Mamlaka ilikadiria kutumia kiasi cha tani milioni moja za
mbolea, na hadi kufikia Januari zaidi ya tani 981,542 sawa na asilimia 91 ya
mahitaji zimeingizwa nchini, huku mbolea nyingine zikiendelea kuingizwa ili
kukidhi mahitaji ya wakulima.
Akizungumza kwa niaba
ya wadau wa tasnia ya mbolea, Wiliam Ngeleja Mjumbe wa Bodi, Kiwanda cha Mbolea
Itracom, ameipongeza Mamlaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na kueleza vikao
vinavyokutanisha wadau wa tasnia hiyo vinaongeza ufanisi katika utendaji wao wa
siku kwa siku.
Aidha mmoja ya wadau
katika kikao hicho Kisarika Nkya Mkurugenzi kutoka MwanaAfrika LDT amesema
msimu huu wapo tayari kuendelea kushirikiana kama wadau ili kusapoti wakulima
wadogo.
Hata hivyo Mkurugenzi
Mtendaji TFRA amesema kuwa mipango yao ni kuhakikisha matumizi ya mbolea katika
maeneo mbalimbali yanapatikana ili kumrahisishia mkulima kufanya kilimo chenye
tija.









