Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.

****************
Na. Mwandishi Wetu, Iringa
Watendaji wa uchaguzi
wametakiwa kuvishirikisha kwa ukaribu vyama vya siasa vyenye usajili kamili
katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi katika maeneo yao ili kurahisisha
utekelezaji wa majukumu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs
Mwambegele leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo
ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma
na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe.
Mafunzo hayo ni sehemu ya
maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Peramiho lililopo
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Kata ya Shiwinga iliyopo
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe unaotarajiwa kufanyika tarehe 26
Februari, 2026.
“Wakati wote wa mchakato wa
uchaguzi huu, ni vema mkavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya siasa vyenye
usajili kamili na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yenu kuhusu masuala
ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia
utekelezaji wa majukumu yenu,” amesema Jaji Mwambegele.
Ameongeza kuwa watendaji hao
wa uchaguzi wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo watakayopewa na
Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Nachukua nafasi hii kuwaasa
kuwa, pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi,
mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa
mazoea. Kwani kila uchaguzi unatofautiana na uchaguzi mwingine,” amesema.
Amewataka watendaji hao kufanya
utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo
husika na kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi
kufanyika kwa utulivu na amani.
Jaji Mwambegele amewasisitiza
watendaji hao kuhakikisha wanaajiri watendaji wa vituo wenye sifa, weledi,
wanaojitambua na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za
kufanya shughuli za uchaguzi.
“Mhakiki vifaa vya uchaguzi
mnavyopokea kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote
vya uchaguzi vinavyohitajika mapema na muweke utaratibu utakaowezesha kila
kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi,” amesema.
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe walikula viapo vya kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Rehema Mayagilo.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamewahusisha
Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa ya Songwe na Ruvuma, Wasimamizi wa Uchaguzi,
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi
ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu.
Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Mhe. Rehema Mayagilo akiongoza viapo vya kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na Kiapo cha kutunza siri kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wakila viapo vya kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kile cha kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Rehema Mayagilo.