Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuhusu madhara ya matumizi holela ya pombe, likilenga kuzuia athari za kiafya na kiuchumi zinazoweza kuwakumba wananchi na familia zao.
Elimu hiyo imetolewa kama sehemu ya jitihada za TBS za kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuimarisha ulinzi wa afya ya jamii kwa kupunguza tatizo la uraibu wa unywaji pombe pamoja na magonjwa yanayotokana na matumizi yasiyo salama ya pombe.
Aidha, wananchi wamehamasishwa kutumia pombe zilizosajiliwa na zinazokidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama ili kujilinda dhidi ya bidhaa hatarishi zisizokidhi viwango.
TBS imeeleza kuwa itaendelea kutoa elimu kwa umma katika mikoa mbalimbali nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi salama ya bidhaa na huduma zinazopatikana sokoni.

