Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Mzee Edwin Isaac Mtei.
Tukio hilo limefanyika nyumbani kwa marehemu Tengeru (Chama), katika Wilaya ya Arumeru Mashariki, Mkoa wa Arusha, leo Januari 24, 2026.
Katika mazishi hayo, Dkt. Mwigulu Nchemba anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo ameshiriki kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na Watanzania kwa ujumla kufuatia msiba wa kiongozi huyo mashuhuri wa kitaifa.
Mzee Edwin Isaac Mtei anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa misingi ya sekta ya fedha nchini, hususan kupitia nafasi yake kama Gavana wa BOT, pamoja na uadilifu na uzalendo wake katika kulitumikia Taifa.

Related
