Mtaalamu wa Mafunzo na Vijana wa Vodacom Tanzania Plc, Bw Samwel Komba (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti Mwanafunzi Anneth Sianga, mhitimu wa programu ya Code Like a Girl, wakati wa mahafali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Ijumaa.
Programu hiyo, inayotekelezwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab, inalenga kukuza uelewa wa wasichana katika ujuzi wa kidijitali ili kuongeza ushiriki wao katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM).
Wengine ni Mkurugenzi wa dLab Dk Mahadia Tunga (kushoto), pamoja na mnufaika wa programu ya Code Like a Girl.



