Na Mwandishi Wetu
WAKAZI na wanariadha wilaya ya Moshi na mkoani Kilimanjaro kwa ujumla wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia uzinduzi wa msimu wa 24 wa mbio maarufu za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2026 uliofanyika hoteli ya Salinero iliyoko Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Yusuf Nzowa aliyewakilishwa na Afisa Michezo wa Mkoa wa Kilimanjaro, Be. Anthony Ishumi, amesema tukio hilo kwa miaka mingi limechangia kwa kiasi kikubwa kuutangaza Mkoa wa Kilimanjaro na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya duniani linapokuja swala la mbio za kimataifa.
“Sote tunajua jinsi mbio za Kilimanjaro Marathon zilizvyochangia ukuaji wa uchumi wa wilaya ya Moshi na Mkoa wa Kilimanjaro kw aujumla kupitia utalii wa michezo”, amesema.
Amebainisha kuwa ukweli kwamba mbio za Kilimanjaro Marathon huvutia zaidi ya washiriki 13,000 na idadi ya watazamaji kutoka zaidi ya nchi 60 duniani kote ambapo alisema katika kuadhimisha msimu wake wa 24 mbio hizo zinakuwa ni kongwe zaidi ya mbio zingine za nyika hapa nchini,” amesema.
“Ninawapongeza wadhamini wote wanaoongozwa na Kilimanjaro Premium Lager (mdhamini mkuu wa mbio za kilomita 42), YAS ambao ni wadhamini wa Kilomita 21 (Kili Half Marathon), Benki ya CRDB ambao ni wadhamini wa mbio za kujifurahisha za kilomita 5, kwa kufanikisha tukio hili”, amesema.
Pia amewapongeza wadhamini wengine ambao alisema ni Pamoja na Kilimanjaro Water, TPC Sugar,GardaWorld Security, Toyota Tanzania, Columbia Sportswear, Simba Cement, Harleys Healthcare Solutions, ALAF Limited, Hoteli ya Salinero,Kibo Palace Hotels ya Jijini Arusha na Keys Hotels a mjini Moshi.
“Pia tungependa kuwashukurumakampuni yatakayofanya maonyesho ya bidhaa wanazozalilsha ikiwa ni sehemu ya tukio hili muhimu; nimetaarifiwa kuwa watafanya maonyesho hayo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha uhsirika Moshi (MoCU) kati ya Machi 21 hadi Machi 23”, amesema .
Ametoa rai kwa washiriki na wale wote watakaokuweko Moshi kipindi chote cha mbio hizi kuwauna mkono wafanyabiashara kwa kutembelea maonyehso hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Khensani Mkhombo, ameeleza kampuni hiyo inajivunia kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo kwa msimu wa 24 mfululizo jambo ambalo alisema limeifanya kampuni hiyo kuwa mdhamini wa muda mrefu kwenye sekta ya michezo kuliko mdhamini mwingine yeyote Hapa nchini Tanzania.
Ametoa rai kwa wale wote wanaotarajia kushiriki bio hizo kujianikisha mapema kupitia ukurasa rasmi ya kujisajili ulioko kwenye tovuti ya www.kilimanjaromarathon.com na pia kupitia Mixx BY YAS.
Kuhusu mbio hizo, Mkhombo alisema zawadi kwa mbio za kilomita 42 zitakuwa ni Sh.5,500,000 kwa washindi wa kwanza kwa washiriki wanaume na wanawake.
“Mshindi wa pili wa kiume na wa kike wanatarajiwa kuzawadiwa Sh.2,800,000,ambapo kwa mshindi wa tatu Zawadi ni Sh.1,450,000.
Awali Mwakilishi wa YAS na MIXX, Bw. Shaibu Hamisi amesema, “YAS inajivunia kwa kuendelea kuwa mdhamini rasmi wa Kilimanjaro International HalfMarathon kwa msimu wa 11; ushirikiano huu unadhihirisha mchango mkubwa unaotolewa na kampuni yetu katika kuwezesha jamii hapa nchini Tanzania”.
Kuhusu zawadi za YAS 21km (Kili Half Marathon) kwa Wanaume na Wanawake alisema kuwa mshindi wa kwanza wa kiume na wa kike watazawadiwa Sh.3,400,000 kila mmoja ambapo mshindi wa pili atapata Zawadi ya Sh.1,700,000 kila mmoja na Mshindi wa tatu atapata Sh.1,200,000.
Wakati huo huo Meneja wa Biashara Kanda ya Kaskazini wa Benki ya CRDB, Bw. Emmanuel Kafui, ambaye benki yake inadhamini mbio za Km 5, amesema, “Iwapo utajiuliza kwa nini Benki ya CRDB inadhamini mbio hizi za Kili Marathon basi jibu ni rahisi tu.
“Ukweli ulio wazi ni kwamba sote hapa tunafahamu kuwa Kili Marathon ni mbio zinazowaleta watu wengi pamoja na ni nyenzo ya kuutangaza utalii wa Tanzania kwani washiriki hutoka ndani ya nchi, Afrika Mashariki, Afrika na duniani kote kwa ujumla.”
Kwa upande wao, waandaaji wa tukio hilo wametoa rai kwa washiriki wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Machi 22, mwaka huu, kufanya usajili wao mapema ili kuepuka changamoto ya kutafuta usajili dakika za mwisho.
Mashindano ya Kimataifa ya mbio za Kilimanjaro Premium Lager, ambayo yatafanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika cha Moshi (MoCU), yameandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon Limited
Ambapo pia kampuni ya Wild Frontiers inawajibika na shughuli zote zinazohusiana na mbio hizo ikiwemo maswala ya usafiri wa ndani Pamoja maswala yote yanayohusiana na masoko Pamoja na matangazo ndani na nje ya nchi.


