Afisa wa Vodacom Tabora Christian Mushanga ( kulia), akikabidhi Kapu la Voda kwa mzazi Modester Kashindye (kushoto) na Mwanafunzi Samwel Paul (katikati).
Tukio hili ni muendelezo wa kampeni ya “Tupo nawe Tena na Tena” ambayo imelenga kugawa makapu kwa wateja wao ambapo msimuu huu unalenga wazazi na wanafunzi wanaorudi mashuleni .
Kampeni hiyo imeendelea kugawa makapu hayo sehemu mbali mbali nchini, na ikilenga kuwaunga mkono wazazi wanaopeleka watoto wao shuleni kwa mwaka mpya wa masomo kwa kuwapa baadhi ya vifaa vya shule vitakavyo wawezesha watoto kuendelea na masomo yao.
Hafla hii imefanyika wilayani Nzega, Mkoani Tabora, Mwanzoni mwa wiki.




