Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia mwanaume mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa Kijiji cha Tingi kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni mke wake ambae pia jina lake limehifadhiwa baada ya kugundua kuwa mwanamke wake anatumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARV).
Akielezea tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma SACP Marco Chilya amesema tukio hilo limetokea January 21, 2026 majira ya saa moja usiku katika kijiji cha Tingi kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma ambapo mwanaume mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa amemjeruhi mke wake kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni baada ya ya kugundua kuwa mwanamke wake anatumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARV) kwa kificho.
Related
