Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuadhimisha siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, siku hii imepewa mwelekeo wa vitendo kwa kusisitiza upandaji wa miti kama ishara ya kuthamini na kulinda mazingira.
Kutokana na ushauri huo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)leo Januari 27,2026 imeungana na Watanzania wengine kuadhimisha siku hiyo kwa kupanda mti, tendo linalobeba ujumbe wa mazingira ni utu na maendeleo endelevu.
Tukio hilo limeongozwa na Ephraim Mafuru, ambapo mti wa matunda umepandwa kuashiria ukuaji na mafanikio yanayoendelea kushuhudiwa katika sekta ya utalii.
Hatua hiyo inaonesha dhamira ya sekta ya utalii katika kulinda mazingira sambamba na kukuza uchumi, huku ikiweka msingi imara wa urithi chanya kwa vizazi vijavyo.







