Mbwambo (34) Ajiua Kwa Kujikata Koromeo Akiwa Geust House – Video



Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa tukio la kifo cha cha Gidion Ebenezeri Mbwambo (34).

Tukio hilo limetokea Januari 27, 2026 katika nyumba ya kulala wageni maarufu kwa jina la Kisanga iliyopo mtaa wa Nguzo kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro. Marehemu alibainika kuwa amekufa baada ya michirizi ya damu na maji kutokeza nje ya mlango wa Chumba namba 106 alichokuwa amepanga.

Baada ya kuvunjwa kwa mlango uliofungwa kwa ndani ilibainika kuwa amekufa akiwa na jeraha la kujikata koromeo la shingo kwa kitu chenye makali.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu amejiua kwa kutumia kitu chenye makali akiwa katika hali ya ulevi, uchunguzi zaidi unaendelea.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kufuata taratibu zote za kuwatambua wageni wanaolala katika nyumba hizo.