Mke Wa Rais Wa Zamani Wa Korea Kusini Ahukumiwa Miezi 20 Jela



Mke wa Rais wa zamani wa Korea Kusini, Kim Koen Hee, amehukumiwa kifungo cha miezi 20 jela kwa kupokea hongo kutoka kwa Kanisa lenye utata la Unification Church.

Mumewe Yoon Suk ambaye ni Rais wa zamani wa nchi hiyo tayari anatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia haki, kuhusiana na jaribio lake la kuweka sheria ya kijeshi mwaka 2024, kitendo ambacho kilimuacha katika hali ya sintofahamu wakati huo.

Ilikuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Korea Kusini kwa Rais wa zamani na mkewe kuhukumiwa na Mahakama kwa wakati mmoja.

Jopo maalum la Majaji walioteuliwa kusikiliza kesi hiyo lilisema Kim alipokea zawadi zenye thamani ya won milioni 80, ikiwa ni pamoja na mkufu wa almasi wa Graff na mikoba kadhaa kati ya Aprili (4) na Julai (7) 2022, kwa malipo ya upendeleo wa kibiashara na kisiasa.

Stori na Elvan Stambuli, Global Digital