OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) CPA.Nicodemus Mkama amesema Mfuko wa Utekelezaji wa Pamoja wa Kampuni ya iTRUST Finance Limited uitwao iTrust EAC Large Cap ETF unakuwa mfuko wa kwanza wenye uwekezaji wa Kikanda unaowekeza kwenye kampuni zenye mitaji mikubwa na zenye utendaji mzuri zaidi kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa Mfuko wa iTRUST EAC LARGE CAP ETF, katika Soko la Hisa la Dar es Salaam leo Januari 28,2026 CPA.Mkama amesema Mfuko wa iTrust EAC Large Cap ETF ni mfuko unaowekeza katika hisa za kampuni zilizoorodheshwa katika masoko ya hisa ya nchi za Afrika Mashariki, ambazo zina mitaji mikubwa na zenye utendaji mzuri zaidi.
“Nawapongeza Bodi na Menejimenti ya iTrust Finance Limited kwa kuwezesha kuweka alama hii kubwa kwenye historia ya Masoko ya Mitaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.”
Amesema pia Mfuko huu unaendeshwa na kampuni ya iTrust Finance Limited ambaye ni Meneja wa Mfuko (Fund Manager) na Benki ya NBC (NBC Bank Limited) ambaye ni Mtunza Dhamana wa Mfuko (Custodian); na umeidhinishwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Amefafanua CMSA ina jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa shughuli katika masoko ya mitaji zinafanyika kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.
“Katika kutekeleza jukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ya mitaji hapa nchini, CMSA huidhinisha uanzishwaji wa bidhaa mpya katika masoko ya mitaji, ikiwa ni pamoja na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja, ambapo katika kutekeleza jukumu hili, Mfuko wa iTrust EAC Large Cap ETF umepata idhini ya CMSA baada ya kukidhi matakwa ya sheria, taratibu na miongozo.
“Mauzo ya vipande vya mfuko wa iTrust EAC Large Cap ETF yamepata mafanikio ya asilimia 540, ambapo kiasi cha Sh. billioni 54.03 kimepatikana, ikilinganishwa na lengo la Sh. bilioni 10,”amesema.
Aidha, asilimia 99.44 ya wawekezaji ni wawekezaji mmoja mmoja yaani Retail Investors na asilimia 0.56 ni wawekezaji ambao Kampuni na Taasisi yaani Institutional investors.Pia amesema asilimia 99.75 ya wawekezaji ni wawekezaji wa ndani na asilimia 0.25 ni wawekezaji wa kigeni.
CPA.Mkama amesema mafanikio hayo yametokana na imani waliyoyano wawekezaji wa ndani na kimataifa kwenye masoko ya mitaji Tanzania na utendaji mzuri wa Kampuni ya iTrust Finance Limited.
Pia ni uthibitisho wa mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kiutendaji yanayotolewa na Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA). Mazingira yaliyowezesha matokeo mazuri ya kihistoria ya Mfuko wa iTrust EAC Large Cap ETF ni pamoja na:
Pamoja na hayo amesema uwekezaji wa Mfuko huo unajumuisha hisa za kampuni za CRDB Bank PLC, NMB Bank PLC, Tanzania Portland Cement Company (Twiga Cement), Tanga Cement PLC.
Nyingine ni Tanzania Cigarette Company Ltd (TCC), Vodacom Tanzania PLC, Safaricom PLC, Equity Group Holdings PLC, KCB Group PLC, British American Tobacco (BAT) Kenya, MTN Uganda Ltd, Stanbic Bank Uganda na Benk ya Kigali. Hatua hii imekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji, kwani utendaji wa hisa hizi una ukwasi na ongezeko la thamani katika masoko husika.
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
