Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF limeufungia uwanja wa KMC kutumika kwenye mechi kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu
Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo imsema:
“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu”.
“Miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu”.
“Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF”.
“TFF inazikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja”.
Timu za Yanga, KMC na Tausi Queens zinapaswa kutafuta viwanja vingine hadi uwanja huo utakapofunguliwa baada ya kufanyiwa maboresho na kukaguliwa upya.