Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamewatembelea Wabunifu na wazalishaji wa majiko ya asili yaliyo boreshwa nakuongezewa bunifu zinazowezesha Nishati Safi (Rafiki Briquettes) kuwaka kwa ufanisi zaidi.
Wakati wa ziara yao, waliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati (REA) Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu. Jackob Kingu ambaye alisisitiza vijana wabunifu kama Jiko Bomba kupewa msaada wa kuongeza ufanisi katika shughuli zao na kufanya uzalishaji wenye tija unaoendana na uzalishaji wa Nishati Safi (Briquettes).
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mha. Hassan Saidy ameahidi kuangalia namna ya wabunifu wa maswala yanayogusa Nishati moja kwa moja hasa vijana kupitia vyuo na sehemu zingine wanafikiwa na wanawezeshwa ili kuongeza idadi ya uzalishaji wa majiko yenye ubunifu na yanayoendana na Agenda ya Taifa ya Nishati Safi 2034.
.jpeg)






