ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kujulisha kuwa limemkamata na linamshikilia Award Karonga, Mkazi wa Katumba ambaye ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Wilaya ya Rungwe na pia ni Makamu Mwenyekiti Hamasa Taifa wa chama hicho.
Alikamatwa Januari 29, 2026 saa 4 asubuhi maeneo ya Mtaa wa Katumba, Kata ya Ibighi – Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwepo uchochezi.
Upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.