…………………
Dodoma
Serikali ya Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Mfuko wa Mazingira Duniani
(Global Environment Facility, GEF) katika ajenda ya maendeleo ya taifa, hususan
katika kuunga mkono juhudi za Serikali za uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu
dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa Dodoma Januari 30,2026 na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Dkt. Richard Muyungi alipokutana na kufanya mazungumzo na Mashirika Wakala
wa Mfuko wa GEF akieleza kuwa kupitia utaalamu, ushirikiano na taasisi za
kitaifa, mipango ya uhifadhi ya Serikali mkono na GEF imeleta manufaa
yanayoonekana ya kimazingira na kijamii na kiuchumi.
“Ushirikiano wetu umewezesha nchi kupata maendeleo makubwa katika
kushughulikia changamoto za mazingira, zikiwemo uharibifu wa ardhi, upotevu wa
bioanuai, athari za mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira.
Ameongeza kuwa mengi yamepatikana chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya
Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hata hivyo, baadhi
ya changamoto zimezidi kuongezeka na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha, kujenga
uwezo wa kitaalamu pamoja ushirikishwa zaidi wa wadau kwa lengo la kupata matokeo
makubwa zaidi.
Dkt. Muyungi amesema Serikali inathamini mchango unaotolewa na mifuko hiyo na iko tayari kushirikiana zaidi
na washirika ili kukusanya rasilimali nyingi zaidi, zinazolingana na ukubwa wa changamoto zilizopo pamoja na matarajio ya
kitaifa na kimataifa za mazingira ya uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi.
“Tunaposonga mbele, Serikali inatoa wito kwa Wizara, Taasisi na Mshirika
wakala wa GEF kutumia nyanja mbalimbali kutoa taarifa ya mafaniko makubwa ya
uhifadhi wa mazingira na maendeleo uliopatikana kutokana na mchango wa Mfuko wa
GEF. Vile vile ni wakati stahiki kwa wadau wote wa GEF kuongeza ushirikishwaji
wa vijana katika utekelezaji wa miradi ya GEF ili kutumia ubunifu na utaalam
walionao ili kuteta faida upande na uhifadhi na ustawi wa jamii kwa kuibua
ajira za kijani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar, Farhat Mbarouk ameshukuru GEF kwa
ushirikiano na Zanzibar kwa kuiwa miradi inayotekelezwa Zanzibar imekuwa chachu
kubwa ya kuongeza juhudi za uhifadh sambamba na jamii kujipatika kipato kwa
shughuli mbadala za kiuchumi ambazo ni rafiki kwa mazingira.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa
ikifanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwa
pamoja na utoaji wa elimu ya Uhifadhi na Utunzaji wa mazingira. Aidha,
Mkurugenzi Farhat alisisitiza umuhimu wa kuongezwa kwa fedha za GEF upande wa
Zanzibar ili kuibua miradi zaidi zaidi ya kuhifadhi mazingira na kuongeza
ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii na sekta za ukuaji wa
Uchumi.

