PSPTB YATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI YA 32, 595 WAMEFAULU, 2 WAMEKAMATWA KWA UDANGANYIFU.


Na Mwandishi wetu Dodoma.

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) iliyoanzishwa mwaka 2007 kwa Sheria ya Bunge Namba 23 ikiwa na Jukumu la kusimamia Taaluma na Wataalam wa ununuzi na Ugavi wa Serikali na Sekta Binafsi

Bodi hiyo huendesha mitihani ya kitaaluma kwa wataalam wa ununuzi na Ugavi katika nafasi tofauti

Bodi hiyo imetangaza rasmi matokeo ya mitihani ya 32 ya PSPTB iliyofanyika Tarehe 01-05 Desemba 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi amesema jumla ya watahiniwa wapatao 1,291 walisajiliwa ili kufanya mitihani hiyo ambapo watahiniwa 1,223 walifanya mitihani hiyo huku Watahiniwa 68 walikosa mitihani husika kwa sababu mbali mbali.

Mbanyi amesema watahiniwa 595 sawa na asilimia 48.7 wamefaulu kati ya Watahiniwa hao 1,223 na watahiniwa 589 sawa na asilimia 48.2 watarudia masomo yao, na Watahiniwa 39 sawa na asilimia 3.2 wamefeli na wataanza upya masomo yao katika ngazi husika.

Aidha Mbanyi amesema Jumla ya Watahiniwa wawili (2) wa ngazi ya CPSP walikamatwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa taratibu za mitihani kwa kuingia ndani ya vyumba vya mitihani wakiwa na karatasi ambazo inasadikika walikusudia kuzitumia kuwasadi kujibu mitihani hiyo.

Bodi ya Wakurugenzi imeielekeza kamati ya usaili na nidhamu kushughulikia suala hilo na wahusika wakikutwa na hatia basi itoe adhabu kali kwa mujibu wa kanuni zilizopo, na matoke ya Watahiniwa hao yamezuiliwa na wahusika wataitwa mbele ya kamati husika ikiwa ni sehemu ya kuwapa haki ya kusikiliza.

Mbanyi ametoa wito kwa Watahiniwa wa mitihani ya PSPTB, wanafunzi wa vyuo na kwa wazazi na watahiniwa waliokosa alama za kutosha kuwafanya wafaulu mitihani hiyo wanahimizwa kujisajili tena na kurudia masomo yao kwenye mitihani iliyopangwa kufanyika mei 2026.

Hata hivyo mbanyi amewataka Watahiniwa wote wa fani ya ununuzi wa Ugavi wajiepushe na vitendo vya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani kwani PSPTB haitasita kuwachukulia hatua kali ili kuhakikisha maadili katika tasnia ya Ununuzi na Ugavi inaenziwa na wadau wote.