Waliokiwasha Taifa Stars waendeleza moto

WALE nyota watatu wa Tanzania waliokiwasha kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), Charles Mmombwa (Floriana FC), Haji Mnoga (Salford City) na Tarryn Allarakhia (Rochdale AFC) wamendelea kukiwasha kwenye klabu zao.

Licha ya Tanzania kuondolewa mapema hatua ya 16 bora, lakini nyota hao watatu wenye asili ya Tanzania walionyesha kiwango bora na kuendelea kuwepo kwenye vichwa vya Watanzania.

Sasa baada ya kumaliza Afcon nyota hao wameendelea kukiwasha wakiwa na timu hizo kwa kuendelea kupewa nafasi ya kuanza kikosini.

Allarakhia anayeitumikia Ligi Daraja la Tatu England tangu ametoka kuitumikia timu ya taifa alicheza dakika 235, dakika 60 dhidi ya Gateshed chama hilo likiondoka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Solihull Moors (77), Rochdale ikishinda bao 1-0, vs Truro (79) ikishinda mabao 2-0.

Mechi nyingine Rochdale ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Southend akicheza kwa dakika 19.

Kwa Mnoga alicheza mechi nne kwa dakika 340, dakika 90 dhidi ya Swindon nyumbani na ugenini, Chesterfield na dakika 70 dhidi ya Bristol Rovers.

Mmombwa anayekipiga Ligi Kuu ya Malta alicheza dakika 75, dhidi ya Hamrun (18) dhidi ya Valleta akicheza kwa dakika 57 chama hilo likitoa sare ya bila kufungana.

Tangu hapo mechi mbili mfululizo hakucheza baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi na Valleta ambayo hakumaliza dakika zote 90.