Na Mwandishi wetu, Amboni Tanga.
Osale Otango ni Paulo Hamisi walikuwa wakifanya kazi katika mashamba ya mkonge mkoani Tanga ambapo mwaka 1952 walitoroka kutoka kwenye himaya ya wakoloni wa kizungu na kwenda kujificha kwenye mapango ya Amboni Tanga kwa ajili ya harakati za kupigania uhuru
Kwa muda wa miaka minne hawakuweza kuonekana na mtu yoyote kutokana na kutumia dawa za asili ambazo ziliwafanya wasionekane na mtu yoyote ingawa walikuwa na uwezo wa kukaa na makundi mengine ya watu ila kutokana na nguvu ya dawa hiyo walikuwa hawaonekani mpaka pale watakapoamua kuaga na kuondoka katika kundi hilo la watu, sharti la dawa hizo walizopewa ilikuwa ni kutofanya zinaa (mapenzi)
Sehemu waliyoishi inapatikana ndani ya mapango ya Amboni Tanga yanayosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo waliweza kuishi katika mapango hayo kwa miaka minne ingawa kuna wakati waliweza kutoka na kwenda maeneo mengine kwa ajili ya harakati za kupigania uhuru lakini kwa nguvu ya dawa waliyopewa watu walikuwa hawawaoni.
Kilichowaponza wawili hao ni kuvunja sharti la dawa kwa kuamua kutoka Amboni na kwenda Lushoto kutafuta mwanamke na kufanya naye mapenzi. Hali hiyo ilitokea mwaka 1956 ambapo mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi na mwanamke huyo nguvu ya nguvu ya dawa ilipotea na kuanza kuonekana na hivyo kukamatwa na kuhukumiwa adhabu ya kupigwa risasi kwa makosa ya kutoroka kwenye mashamba ya mkonge kwenda kwenye harakati za kupigania uhuru.
Kukiuka masharti hayo inaenda sambamba na usemi usemao “asiyesikia la Mkuu huvunjika guu”na ukiambiwa zinaa mbaya ndiyo uelewe na ndiyo maana baadhi ya vitabu takatifu vinatufundisha kuwa usikaribie zinaa na ukimuangalia mke wa mwenzio kwa jicho la kumtamani basi umezini, Karibuni mapango ya Amboni mujionee mahali walipokuwa wakiishi jamaa hao wawili.

