WAFANYAKAZI TUME YA UTUMISHI WA UMMA, WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA NGORONGORO.

Watumishi wa ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma, leo Februari 4, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisa H. Kalombola, wametembelea  hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya utalii wa ndani, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, uliofanyika jana Februari 3, 2026.