Baadhi ya waandishi wa habari Mkoani Iringa wamepata ajali leo Feb 5, 2026 wakati wakitoka kwenye sherehe za Maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo yamefanyika kimkoa katika Kata ya Idodi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Taarifa zilizotufikia hivi punde gari lililopata ajali aliyokuwepo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Mkoa wa Iringa Joseph Nzala Lyata, Frank Leonard Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa ambaye pia ni mwandishi wa Magazeti ya serikali, Denis Mlowe kutoka fullshangwe blog ,Clement Sanga wa Channel Ten, Herieth Mola wa Mkombozi Online Tv pamoja na Zuhura Zukheri wa Abood Tv Taarifa zaidi tunaendelea kufuatilia kujua idadi ya majeruhi lakini hakuna kifo chochote kilichotokea.
Chanzo : Nuru Fm