Askari Kutoka Tanzania wavishwa nishani kutambua mchango wa kulinda Amani Sudan Kusini.

Maafisa,na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi Nchini Tanzania ambao nikundi lilomaliza muda wake wa kuhudum kulinda amani nchini Sudan kusini wamehitimisha kwa Paredi maalum ambayo ili ambatana na kuwavisha nishani( Medall Pin) maafisa na askari hao ikiwatambua kwa kazi nzuri ya kudumisha amani.

Tanzania ni miongoni mwa nchi bora zinazochangia askari wake katika Operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Aidha Miongoni mwa maafisa hao wamebainisha kuwa licha ya kuwa mazingira magumu ya iliwapa moyo kuendelea kulinda amani na kutoa elimu kwa makundi mengi zaidi.

Sambamba na hilo wameendelea kuwashukuru maafisa wengine wa majeshi kwa namna walivyoshirikiana kudumisha amani katika misheni ya kulinda amani nchini Sudan Kusini

Mwisho wamewaomba wananchi wa Sudan kusini kuendelea kutunza na kulinda amani ya nchini hiyo.