KOCHA wa Bunda Queens, Alley Ibrahim amesema tofauti ya ubora kati ya timu nyingi imekuwa ndogo msimu huu jambo linaloongeza ushindani.
Bunda iko nafasi ya nane na pointi tisa kwenye mechi 11 imeshinda tatu na sare nane ikifunga mabao 11 na kuruhusu mabao 27.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ibrahim amesema ongezeko la timu mbili limeongeza ushindani kwenye ligi na kwamba ushindani huo umechangia kuongeza hamasa kwa wachezaji na mashabiki.
Alley amesema kila timu inapambana kuhakikisha inapata matokeo chanya, hali inayofanya kuwa na mechi ngumu.
Kocha huyo alifafanua kwa kusema, mzunguko wa pili watafanya maandalizi kwa umakini mkubwa na kwamba benchi la ufundi limepitia mapungufu yaliyopo ili kuyarekebisha kabla ya kurejea kwa ligi.
“Adhabu ya kupokwa pointi iliturudisha nyuma lakini hatuko nafasi mbaya mzunguko wa kwanza umekwisha tunajipanga na wa pili kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri kwetu,” amesema Ibrahim.