Dar es Salaam. Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waibua shangwe baada ya mwenyekiti wao, Tundu Lissu kupandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam ambapo kesi ya uhaini inayomkabili inatarajiwa kuendelea kuunguruma leo, Februari 9, 2026.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka utajibu hoja za kisheria za pingamizi la Lissu kuhusiana na uhalali wa mashahidi fiche wa Jamhuri.
Lissu alivyopandishwa kizimbani Mahakama Kuu
Kesi imepangwa kuanza tena leo kwa siku 20 mfululizo za kazi, mpaka Machi 6, 2026.
Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini, kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi