Rais Mstaafu Dkt Kikwete Akabidhiwa Nakala ya Kitabu cha Plato

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea nakala ya kitabu “Jamhuri na Plato” kilichotafsiriwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka kwa Bw. Walter Bgoya, Mkurugenzi wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota, mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Kitabu hiki, asili yake ikiwa ni The Republic (Politeia) cha mwanafalsafa wa Kigiriki Plato, kinajadili mazungumzo ya Socrates, ambapo Plato anachambua aina za tawala, asili ya nafsi, nadharia ya maumbo na dhana ya mji bora (Kallipolis) unaoongozwa na wanafalsafa-wafalme.
Tafsiri hii ya Mwalimu Nyerere inaleta fikra hizi karibu na muktadha wa Afrika, ikisisitiza maadili, uongozi wenye hekima na wajibu wa raia katika kujenga jamii bora.
Dkt Kikwete alikabidhiwa pia nakala ya vitabu vya wasifu na hotuba vya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa.