LUGANGIRA AKUTANA NA MTENDAJI WA TUME YA UMOJA WA MATAIFA YA UCHUMI KWA AFRIKA

Katibu Mkuu wa Women Political Leaders (WPL), Neema Lugangira, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Claver Gatete, Katibu Mtendaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (United Nations Economic Commission for Africa).

Wawili hao wamejadiliana kuhusu mchango wa lishe katika maendeleo ya kiuchumi na umuhimu wa Serikali za Afrika kuipa lishe uzito wa kimkakati sawa na sekta nyingine za ukuaji.

Pia, wameangazia jinsi teknolojia za kidijitali na teknolojia mpya kama akili mnemba AI zinavyoweza kuharakisha maendeleo; na nafasi ya viongozi wanawake katika kuongoza ajenda hii hivyo kuchangia ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Wamekutana leo jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia.