Mshikamano wa viongozi wa sekta ya afya umeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kuongeza ufanisi wa usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za chanjo, hatua inayolenga kuhakikisha kila mtoto anayestahili anapata chanjo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 13,Februari 2026 Mkoani Tabora wakati kufunga Mafunzo ya Wasimamizi wa Ngazi ya Kati (MLM) ambapo viongozi walisisitizwa kuimarisha uratibu, usimamizi na matumizi ya takwimu katika kufuatilia utekelezaji wa huduma za chanjo kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Halmashauri.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mratibu wa Chanjo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Dkt. Florian Tinuga, amesisitiza kuwa uhamasishaji kupitia mikutano ya vijiji na mitaa pamoja na elimu inayotolewa na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) ni nyenzo muhimu ya kuongeza mwitikio wa jamii kuhusu chanjo.
Aidha, ameeleza kuwa usimamizi madhubuti wa mnyororo baridi (cold chain) na matumizi sahihi ya takwimu katika kupanga na kufuatilia huduma ni hatua muhimu za kuboresha ubora na ufanisi wa chanjo.
Kwa upande wake, Simon Nzilibili kutoka Wizara ya Afya amehimiza viongozi kuendelea kuunganisha nguvu, kuimarisha uwajibikaji na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa shughuli za chanjo katika maeneo yao.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora amepongeza mafunzo hayo, akisisitiza umuhimu wa kuweka kipaumbele katika bajeti za chanjo na kuimarisha rasilimali ili kuhakikisha usimamizi na ufuatiliaji wa huduma hizo unakuwa endelevu na wenye tija kwa jamii.
“Uhamasishaji kupitia mikutano ya vijiji na mitaa pamoja na elimu kupitia redio za kijamii, Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) ni nyenzo muhimu ya kuongeza mwitikio wa jamii kuhusu chanjo”amesema.
Aidha, ameeleza kuwa usimamizi madhubuti wa mnyororo baridi (cold chain) na matumizi sahihi ya takwimu katika kupanga na kufuatilia huduma ni hatua muhimu za kuboresha ubora na ufanisi wa chanjo.
Kwa upande wake, Simon Nzilibili kutoka Wizara ya Afya amehimiza viongozi kuendelea kuunganisha nguvu, kuimarisha uwajibikaji na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa shughuli za chanjo katika maeneo yao.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutanisibwa amepongeza mafunzo hayo, akisisitiza umuhimu wa kuweka kipaumbele katika bajeti za chanjo na kuimarisha rasilimali ili kuhakikisha usimamizi na ufuatiliaji wa huduma hizo unakuwa endelevu na wenye tija kwa jamii.