FCC YAING’ARISHA TANZANIA KATIKA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA BIASHARA DUBAI

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Bi. Khadija Ngasongwa,akitoa maelezo namna FCC inavyoshirikiana na wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji wa mizigo (logistics) katika kuongeza thamani kwenye biashara, ushindani na uwekezaji nchini Tanzania wakati wa kongamano la kimataifa la biashara na sekta ya usafirishaji wa mizigo (Tanzania Trade & Logistics Forum) liliofanyika Februari 13 – 14, 2026 katika Hoteli ya Shangri-La, Dubai, UAE

📍 Dubai, UAE

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, wameshiriki kimkakati katika Kongamano la Kimataifa la Biashara na Sekta ya Usafirishaji wa Mizigo (Logistics) lililofanyika jijini Dubai, Falme za Kiarabu.

Lengo la kongamano hilo ni kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kuongeza fursa za biashara kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu, sambamba na kufungua masoko mapya kwa bidhaa na huduma za Tanzania.

Akizungumza katika kongamano hilo kama mgeni rasmi, Mhe. Dennis Londo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya usafirishaji  ili kuongeza ufanisi katika upanuzi wa masoko, kukuza mauzo ya nje, na kujenga ushirikiano wa kimataifa wenye tija kwa Taifa.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bi. Khadija Ngasongwa, alisema kuwa Tume ya Ushindani inaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza biashara kwa kasi na ufanisi. Alieleza kuwa sekta ya usafirishaji wa mizigo ni mhimili muhimu katika kuongeza thamani kwenye biashara na uwekezaji nchini.

“Tutaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa ushindani sokoni ili kuchochea ukuaji wa biashara na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha biashara na huduma za usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,” alisisitiza.

Kongamano hilo limejumuisha Taasisi za Serikali, wawekezaji na watoa huduma wa Tanzania ambapo washiriki wamepata fursa ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu ya fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya usafirishaji. 

Waandaaji wa kongamano hilo ni TANFORD, jukwaa linalowaunganisha wamiliki wa kampuni za Kitanzania zinazojihusisha na mizigo na usafirishaji wanaofanya shughuli zao Dubai na katika masoko ya kimataifa.

Kongamano hilo limefanyika tarehe 13 – 14 Februari, 2026 katika Hoteli ya Shangri-La, Dubai, UAE ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja za serikali na sekta binafsi katika kulinda na kukuza maslahi ya Taifa katika biashara Duniani.

 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo (Mb),akizungumza na wafanyabiashara na wadau wa sekta ya usafirishaji (logistics) wakati wa kongamano la kimataifa la biashara na sekta ya usafirishaji wa mizigo (Tanzania Trade & Logistics Forum) Februari 13, 2026 katika Hoteli ya Shangri-La, Dubai, UAE.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Bi. Khadija Ngasongwa,akitoa maelezo namna FCC inavyoshirikiana na wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji wa mizigo (logistics) katika kuongeza thamani kwenye biashara, ushindani na uwekezaji nchini Tanzania wakati wa kongamano la kimataifa la biashara na sekta ya usafirishaji wa mizigo (Tanzania Trade & Logistics Forum) liliofanyika Februari 13 – 14, 2026 katika Hoteli ya Shangri-La, Dubai, UAE

Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini kongamano la kimataifa la biashara na sekta ya usafirishaji wa mizigo (Tanzania Trade & Logistics Forum) lililofanyila Februari 13 – 14, 2026 katika Hoteli ya Shangri-La, Dubai, UAE