TCB Selous Marathon kutikisa mkoa wa Morogoro Juni 20

Mwandishi Wetu,Mwananchi

Benki ya TCB  imetangaza msimu wa nane wa mbio za nyika TCB Selous Marathon kufanyika Juni 20 mwaka huu lengo kutengeza jamii yenye afya bora.Mbio hizo zitakazofanyika mkoani Morogoro zikiwa na kaulimbiu ya ‘Mzuka zaidi’itahusisha umbali wa Km5, Km10 na Km 21.

Mwakilishi wa TCB kutoka Kurugenzi ya Fedha Neema Saimon akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam  amesema TCB marathon itakuwa zaidi ya mbio na harakati za kutengeneza maisha bora kwa jamii.“TCB tunahamaisha zaidi mazoezi na tunapenda kuhudumia jamii yenye afya bora, mbio hizi zitasaidia kukuza utalii kutokana n jina la Hifadhi pamoja kuchochea   maendeleo ya nchi,”amesema.

Kwa upande wake amesema Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya TCB Selous Marathon Imani Kajula amesema TCB kujiunga katika mbio za Selous Marathon ni kuongeza chachu ya kukuza afya na biashara.

Amesema kwa muda ambao mbio hizo hufanyika mkoa wa Morogoro huchangamka.

kwa washiriki,Kajula amewataka kufahamu TCB imeshiriki katika ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR kifedha.

“Sisi Selous Marathon tunachofanya ni kuwezesha watu kusafiri kwa haraka sana.

“Lengo letu tumekuwa mbio tunaozingatia vigezo na benki nanyi tunaamini mnazingatia vigezo, tunasimama hapa hatudaiwi na vyama vyovyote vya michezo tunafuata sheria zote za uendeshaji wa mbio na wakimbiaji wote wanaoshiriki hawatudai,”amesema

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo na wakati benki ya TCB, Lilian Mtali amesema TCB imepata hati rasmi ya kutumia jina la Selous Marathon kuwa TCB Selous Marathon.

“Haya si mabadiliko ya jina pekee bali kuboresha thamani na uzoefu wa washiriki kama benki imejipanga kuongeza thamani na kuimarisha maandalizi ili wakimbiaji wapate uzoefu na fursa zaidi, kwa kuwa TCB ina matawi nchi nzima itakuwa raisi kwa wakimbiaji kupata vifaa vya mbio,”amesema.

Amesema wameamua kushirikiana na Selous Marathon ili kuonyesha taswira ya benki yao kuwa inahudumia wateja wa aina zote bila kujali wanakotoka.

Lilian amesema watu wote watakaohitaji kushiriki mbio hizo, watafikiwa kwa haraka kupitia matawi yao yaliyopo nchi nzima.Kwa upande wake Katibu wa chama cha riadha mkoa wa Morogoro Omari Mohammed amesema wamejipanga kuhakikisha usalama wa wakimbiaji wa mbio hizo huku akiwaomba wanariadba kuchukua tahadhari na kuwa makini wawapo barabarani.

“Pamoja na marathon nyingi kufanyika vizuri wananchi wa Morogoro walishukuru zaidi kuwepo kwa mbio mwaka jana, naomba niwape tahadhari mwaka huu mnapokuja Morogoro kusiwe na mtu anatembea peke yake kuna watu wanaitwa vishandu haw ani watu wanaopenda kupora vitu kwahiyo mnapotembea mtembee kwa vikundi,”amesema Selous Marathon imepangwa kufanyika Juni 20 mwaka huu mjini Morogoro ukiwa na msimu wa unaojirudia kufanyika  tangu kuanzishwa kwa mbio hizo.