-Pia awasilisha Salamu za Pole za Rais Dkt. Samia kwa waliofariki kwenye Machimbo, Korogwe.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amehani msiba wa Idrissa Zubeir Bin Ali (58) ambaye ni mdogo wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally ambae amefariki Februari 15, 2026 katika Hospitali ya Muhimbili Dar Es salaam.
Akiwa Msibani hapo kuhani msiba huo, Mhe. Dkt. Mwigulu amewasilisha salamu za pole kwa wanakorogwe kutoka kwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vifo watu watano vilivyotokea Februari 15, 2026 katika Machimbo ya Mchanga ya BOLBIT kijiji cha Makuyuni, Tarafa ya Mombo.
“Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anawapa pole na kuwaombea moyo wa subira ndugu, Jamaa na wafiwa na Mwenyezi Mungu awape Pumziko la Amani marehemu wote”.

