Mzee Hiza Wa ‘Tanzania Yetu’ Afariki Dunia



Msanii mkongwe wa muziki Tanzania, Mzee Hiza, mtunzi na mwimbaji wa wimbo maarufu wa “Tanzania Yetu”, amefariki dunia.

Mzee Hiza alikuwa maarufu kwa kutunga na kuimba wimbo Tanzania Yetu – Nchi ya Furaha ambao umekuwa ukielezea uzalendo na umoja wa Watanzania kwa miaka mingi.

Wimbo huo aliuandika akiwa na Bendi ya Atomic Jazz ya Tanga mwaka 1966/1967 na umechukua nafasi muhimu katika utamaduni wa muziki wa Tanzania.