BAADA ya kung’olewa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya ushindi wa kishindo wa mabao 3-0 mbele ya JS Kabylie ya Algeria, Yanga inarejea mzigo kuanza utetezi wa taji la Kombe la Shirikisho CRDB ikikabiliana na mabingwa wa zamani wa Tanzania, Cosmopolitan.
Yanga inalishikilia taji la michuano hiyo ambayo iliasisiwa mwaka 1967 ikiwa kwa jina la Kombe la FAT kabla ya kuitwa Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa misimu minne mfululizo, na inakutana na Cosmo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Bara mwaka 1968 na kuwa timu ya kwanza kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya CAF, japo ilijitoa mwan-zoni mwa michuano.
Watetezi hao wataanza rasmi kampeni ya kutetea taji hilo leo Jumatano kwenye Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam, huku ikijua inakutana na timu kongwe yenye rekodi zake nchini.
Yanga, ambao ni mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ikitwaa mara tisa, ikiwamo kubeba kwa misimu minne mfululizo iliyopita, inataka kumaliza hasira za kutolewa CAF kwa kukabiliana na Cosmopolitan iliyopo Ligi Daraja la Pili (First League) kwa sasa.
Licha ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Kabylie ya Algeria katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, timu hiyo ilishindwa kutinga hatua ya robo fainali ikiwa ni msimu wa pili mfululizo.
Yanga ilikuwa inahitaji ushindi wa zaidi ya mabao 3-0 kama huo ilioupata, ingawa hesabu za kikosi hicho za kufuzu robo fainali zilififia, baada ya washindani wake, AS FAR Rabat ya Morocco, kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Suluhu hiyo ya AS FAR Rabat iliifanya timu hiyo kufikisha pointi tisa katika kundi B, ikiungana na Al Ahly iliyoongoza na pointi 10, huku Yanga ikimaliza ya tatu na pointi zake nane, wakati JS Kabylie ikiburuza mkiani na pointi tatu tu.
Kwa sasa malengo ya timu hiyo ni kutetea mataji yote ya ndani iliyoyachukua, ikiwemo Ligi Kuu Bara na Kombe hili la FA, inaloanza kutupa karata yake upya katika hatua ya 64 bora, ambalo hutoa mwakilishi wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Rekodi zinaonyesha kuwa Yanga haijapoteza mechi ya Kombe la Shirikisho tangu Julai 25, 2021, ilipofungwa katika fainali ya msimu wa 2020-2021 kwa bao 1-0 na watani wao wa jadi, Simba, pambano likipigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma.
Hata hivyo, kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema hataidharau Cosmo kwa kutambua mechi za FA huwa na ma-tokeo ya kustaajabisha na lengo la timu ni kupata matokeo na kutetea taji kwa mara ya tano mfululizo sambamba na Ligi Kuu Bara, hivyo wataingia uwanjani kwa umakini.
Mbali na mechi hiyo, leo pia kuna mitanange mingine itapigwa ikiwamo ile ya Mashujaa dhidi ya Nkim ya Tanga kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, huku jijini Mwanza kukipigwa ‘Derby’ itakayovuta hisia za wadau wengi, itaka-yozikutanisha Pamba Jiji dhidi ya Alliance FC.
Mabingwa wa taji hilo kwa msimu wa 2017-2018, Mtibwa Sugar, itakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma kuikari-bisha IAA SC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili kutoka Arusha, huku maafande wa JKT Tanzania wakiikaribisha Pan Africans kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano 1998, African Sports, itaikari-bisha Kilimo ya mkoani Singida, huku Stand United ‘Chama la Wana’ ikikabiliwa na ‘Derby’ ya Shinyanga dhidi ya ma-bingwa wa Mkoa huo, Mabao FC.
Hausung ya Njombe itaikaribisha West Singers ya Mwanza, wakati maafande wa Polisi Tanzania watakuwa Ushirika mjini Moshi kucheza na THB FC ya Rukwa, huku Bigman ya Lindi ikiwa kwenye Uwanja wa Ilulu kucheza na kikosi cha Nyika FC ya Pwani.
Songea United itaikaribisha Mabingwa wa Mkoa wa Njombe, Vijana SC kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma, wakati Mbuni FC ya Arusha itacheza dhidi ya The Green FC ya Songwe, huku Barberian FC ya Dar es Salaam ikicheza na Kijiwe Nongwa ya Songwe.
B19 FC, zamani Tanesco inayoshiriki Ligi ya Championship, itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Dhujau FC ya Katavi, wa-kati KenGold ya Mbeya itaikaribisha Magereza ya Dar es Salaam, huku Mbeya Kwanza ikicheza na FGA Talents ya mkoani Morogoro.
YANG 03
Kagera Sugar itakuwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kucheza dhidi ya Mighty Elephant ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Ruvuma, huku vinara wa Championship msimu huu, Geita Gold yenye pointi 46, ikiikaribisha Kajuna FC ya Kigoma.
Bingwa wa michuano hiyo uwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo kwa msimu huu Azam FC na Sin-gida BS zilipata nafasi hiyo na kutinga makundi kwa mara ya kwanza, licha ya zote kukwama kwenda robo fainali kama ilivyokuwa kwa Yanga na Simba zilizoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni rekodi kwa Tanzania kuingia timu nne hatua ya makundi ya CAF.