MBUNGE WA MOSHI MJINI ANUSURIKA KIFO , AJALI YA GARI


 ::::::::

Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Ibrahimu Shayo, amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupinduka mara kadhaa na kutumbukia korongoni katika eneo la Kirinjiko, Wilaya Same, mkoani Kilimanjaro. 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ajali hiyo ilitokea wakati akiwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba.

 Msafara huo ulitokea Same kuelekea Wilaya ya Mwanga. 

Hata hivyo inadaiwa Mbunge huyo hakuonekana katika eneo la Mwanga ambako Waziri Mkuu alikuwapo. Tunaendelea kuwatafuta Jeshi la Polisi, kwa habari zaidi. 

Chanzo : Nipashe Digital