Wasira Amtembelea Mama Maria Nyerere Msasani – Global Publishers



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara), Stephen Wasira, Februari 18, 2026 amemtembelea na kumjulia hali Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam.

Mama Maria ni mjane wa Hayati Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania, ambaye aliongoza nchi katika misingi ya umoja, amani na maadili ya uongozi.

Ziara hiyo inaelezwa kuwa ni ya heshima na kujuliana hali, ikionesha kuthamini mchango wa familia ya Mwalimu Nyerere katika historia ya taifa.