Kamanda Mkuu wa Waasi wa M23 Auwawa Katika Shambulio la Drones Mashariki mwa DRC

Global Publishers
February 25, 2026
0 Comments

Kamanda wa juu wa kundi la waasi la M23, Lieutenant-Colonel Willy Ngoma, ameuawa mapema Jumanne katika shambulio la drones karibu na Rubaya, jimbo la North Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Tukio hilo lilitokea majira ya saa 9 usiku GMT (3:00 a.m. muda wa eneo).

Rubaya ni mji muhimu kiuchumi, ukitoa takriban asilimia 15 ya coltan duniani, rasilimali muhimu katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki. Eneo hili limekuwa kikomo cha mapambano kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali.

Shambulio hilo limetokea wakati wa juhudi za kuweka mapumziko ya mapigano (ceasefire), zenye usimamizi wa kimataifa zikiwemo za Qatar, Umoja wa Afrika, na Marekani.