Saleh Aipa Moyo Simba Kabla ya Dabi ya Kariakoo ‘Wajiamini’ – Video

Global Publishers
February 27, 2026
0 Comments

Mchambuzi nguli wa soka nchini, Saleh Jembe, amesisitiza kuwa hakuna sababu kwa Simba kuiogopa Yanga Machi 01, 2026 katika dimba la New Amaan Complex visiwani Zanzibar, maarufu kwa jina la utani Guantanamo Bay.

Kwa mujibu wa Jembe, mechi kati ya Simba na Yanga ni ya ushindani wa kihistoria ambapo maandalizi, mbinu za makocha na ari ya wachezaji ndivyo vinavyoamua matokeo si hofu wala presha ya jina la mpinzani.

Ameongeza kuwa Simba ina kikosi chenye uzoefu na uwezo wa kushindana katika mechi kubwa, hivyo inapaswa kuingia uwanjani kwa kujiamini na kutafuta ushindi.

Dabi ya Kariakoo imekuwa na ushindani mkubwa kwa miaka mingi, ikipewa uzito mkubwa na mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.