Waumini Wajitokeza Kumuaga Kardinali Pengo Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu – Video

Global Publishers
February 27, 2026
0 Comments

Waumini na viongozi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa Polycarp Pengo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam.

Ibada ya kuaga imeambatana na huzuni, vilio na sala maalum za kumuombea marehemu, huku waumini wakikumbuka mchango wake mkubwa katika kuliongoza Kanisa Katoliki na kulihudumia taifa kwa ujumla.

Viongozi wa dini na serikali walihudhuria kutoa heshima zao za mwisho, wakieleza kuwa Kardinali Pengo ameacha alama isiyofutika katika historia ya Kanisa na jamii.

Ibada na shughuli za mazishi zinaendelea kwa ratiba iliyotangazwa na Kanisa.